LADY JAY DEE AZINDUA MAJI YENYE JINA LAKE
MWANAMUZIKI
wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura (Lady Jay Dee) pichani, mapema
leo amezindua maji yenye jina lake katika hafla ilifanyika Paradise City
Hotel, jijini Dar es Salaam. Akiongea katika uzinduzi huo, Jay Dee
alisema kwamba, anatarajia kuyaingiza maji hayo mtaani kuanzia Januari
Mosi, 2011, na yatauzwa kwa bei ya kawaida. Alielezea pia namna
atakavyoendesha shughuli zake za kibiashara na sanaa kwa ujumla.
Akifafanua zaidi, alisema bendi yake itapunguza shoo ambapo sasa atapiga
siku moja tu kwa wiki tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Maonyesho
hayo yatakuwa yakifanyika kila siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Mzalendo
Pub Millennium Tower Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Pia Jay Dee,
ambaye anakuwa mwanamuziki wa kwanza nchini kuwa na jina kwenye bidhaa
kama maji, aligusia sula la kufanya kazi za kimataifa zaidi, likiwemo la
kuingia mkataba na kampuni ya Rock Star, ambayo itasimamia kazi zake za
muziki kwa muda wa miaka mitano.
Alimalizia
kwa kusema kuwa mwanzoni mwa mwaka ujao, anatarajia kufungua mgahawa
wake mkubwa maeneo ya Kinondoni-Morocco jijini Dar es Salaam, ikiwa ni
moja ya mipango yake ya kimaendeleo kwa mwaka 2011.
Maji yaliyozinduliwa yakionyesha lebo yenye jina la Lady Jay Dee, muda mfupi kabla ya mchakato huo kuanza.
..maji na matamu!
Mwakilishi wa MTV na Rock Star Tanzania, Christine Mosha ‘Seven’ akifafanua jinsi mkataba wa JayDee na kampuni hiyo ulivyo.
Mpiga picha wa kampuni ya Habari Corporation, Muhidin Sufiani, akitimiza wajibu wake katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki
wa Bongo Fleva, Jaffary Mshamu ‘Jaffaray’ (katikati), akiwa kwenye pozi
na baadhi ya wadau waliofika kushuhudia uzinduzi huo.
Mwanamitindo Fideline Iranga (kushoto), akiwa kwenye pozi na mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata, muda mfupi baada y
No comments: