Jinsi Ya Kuandika Andiko La Mradi
Tuesday, December 17, 2013 | Posted by Unknown
Andiko la Mradi ni maelezo yanayoelezea mradi husika
kwa kujibu maswali ya vihatarishi vya mradi, fursa zilizopo, rasilimali
na jinsi vitakavyotumika, mpangilio mzima wa kuutekeleza mradi ikiwa ni
pamoja na uongozi na usimamizi, mpango endelevu wa mradi kwa hapo
baadaye kwa upande wa kitaasisi na kifedha
Mradi huo unaitwaje?, Utakuwa maeneo gani?, Unafanyika kwa muda
gani?, bajeti yake ni kiasi gani?, Wafadhili wa mradi ni akina nani?,
Namba ya mradi kama ipo na kipindi cha kuanza na kumalizika kwa mradi.
Maswali mengine ni kama ifuatavyo; Historia ya tatizo lililo
sababisha mradi kuwepo ni ipi?, Mradi huu umetokana na serikali, mtu
mmoja au jamii na ulianzaje au wazo lilianza nkwa nani?
Kwanini tuwe na mradi huu katika jamii hii kipindi hiki?, Je, mradi
ni suluhisho halisi na sahihi la tatizo hilo?, Je unadhani kama
hautatekelezwa kwa sasa mradi huu utaleta madhara yoyote? Kuna ulazima
wowote wa kuufadhili mradi huu?
Unaweza kusema kwa ufupi mradi huu hasa unashughuli zipi na unatekelezwaje katika jamii hii.
Utasimamiwa na nani au watu wangapi na kwa nafasi zipi kwa njia gani
hasa ili kuwafikia jamii?, Je mradi huu utahusisha watu wangapi
kiutendaji na pia utawalenga watu kiasi gani na wanawake wangapi na
waume wangapi?
Malengo au Lengo kuu la mradi ninini? Madhumuni yake mengine ni
yapi? Shughuli za mradi na majukumu madogomadogo ninini? Ambayo lazima
yapangwe kimantiki na kwa matarajio yenye kufikia lengo.
Ni wadau wangapi na watashiriki vipi katika kufanikisha mradi huu,
mchango wa wadau hao unamasharti yoyote yanayoweza kuathiri mradi huu ?
Kuna uhusiano wowote kati ya mradi huu na maswala ya kijinsia? Swala
la mazingira linaingia wapi katika mradi huu? Swala la Ukimwi na
magonjwa yasiyotibika yanasehemu gani katika matokeo na utekelezaji wa
mradi huu?
Umepanga kuitekeleza vipi tathimini na ufuatiliaji wa shughuli za
mradi huu? Uendelevu wake na bajeti vimegusa maeneo yote ya mradi huu
kwa namna gani?
Swali linguine ni kama kuna mradi kama huu uliowahi kutekelezwa hapo au jirani na hapo katika kipindi kifupi kilichopita.
How about this Article
No comments: